Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mikali
1 Samweli 18 : 28
28 Sauli akaona na kutambua ya kwamba BWANA alikuwa pamoja na Daudi; na huyo Mikali, binti Sauli, akampenda.
1 Samweli 19 : 17
17 ⑤ Sauli akamwambia Mikali, Mbona wewe umenidanganya hivi, na kumwacha adui yangu aende, hata ameniponyoka? Naye Mikali akamjibu Sauli, Yeye aliniambia, Niache niende zangu; kwa nini nikuue?
1 Samweli 25 : 44
44 ⑲ Lakini Sauli alikuwa amemposa Mikali, binti yake aliyekuwa mkewe Daudi, kwa Palti, mwana wa Laisha aliyekuwa mtu wa Galimu.
2 Samweli 3 : 16
16 Huyo mumewe akafuatana naye, huku akilia, akamfuata mpaka Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia, Haya, rudi. Naye akarudi.
2 Samweli 6 : 16
16 Ikawa, sanduku la BWANA lilipoingia mji wa Daudi, Mikali binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele za BWANA; akamdharau moyoni mwake.
2 Samweli 6 : 23
23 Basi Mikali, binti Sauli, hakuwa na mtoto hata siku ya kufa kwake.
Leave a Reply