Biblia inasema nini kuhusu Mfungwa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mfungwa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mfungwa

Mwanzo 14 : 12
12 ⑳ Wakamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao.

1 Samweli 30 : 2
2 ⑲ nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wowote, ila wakawachukua, wakaenda zao.

Hesabu 31 : 20
20 Na kuhusu kila nguo, na kila kitu kilichofanywa cha ngozi, na kazi yote ya singa za mbuzi, na vyombo vyote vilivyofanywa vya mti, mtajitakasa wenyewe;

Kumbukumbu la Torati 20 : 13
13 na BWANA, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga;

Kumbukumbu la Torati 21 : 10
10 ⑤ Utakapokwenda vitani kupigana juu ya adui zako, na BWANA, Mungu wako, awatiapo mikononi mwako, nawe uwachukuapo mateka,

Yoshua 8 : 29
29 Na huyo mfalme wa Ai akamtundika katika mti hadi wakati wa jioni; kisha hapo jua lilipokuchwa Yoshua akaagiza, nao wakauondoa mzoga wake katika huo mti, na kuutupa hapo penye maingilio ya lango la mji, kisha wakaweka pale juu yake rundo kubwa la mawe, hata hivi leo.

Yoshua 10 : 40
40 ③ Basi Yoshua akaipiga nchi hiyo yote, nchi ya vilima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela, na nchi ya materemko, na wafalme wake wote; hakumwacha aliyesalia hata mmoja; lakini akawaharibu kabisa wote waliokuwa hai, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.

Yoshua 11 : 11
11 Nao wakawapiga wote pia waliokuwamo ndani ya Hazori kwa makali ya upanga, wakawaangamiza kabisa; hakubakizwa hata mmoja akiwa hai; kisha akauteketeza Hazori kwa moto.

Waamuzi 7 : 25
25 ⑰ Wakawashika hao wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu; wakamwua huyo Orebu pale penye jabali la Orebu, na huyo Zeebu wakamwua hapo penye shinikizo la divai la Zeebu, kisha wakawaandamia Wamidiani; vichwa vya Orebu na Zeebu wakamletea Gideoni huko ng’ambo ya pili ya Yordani.

Waamuzi 8 : 21
21 Ndipo hapo Zeba na Salmuna wakasema, Simama wewe utuue sisi; kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Basi Gideoni akasimama, akawaua Zeba na Salmuna, akazitwaa koja zilizokuwa katika shingo za ngamia wao.

Waamuzi 21 : 11
11 ④ Na jambo mtakalotenda ni hili; mtamwangamiza kila mwanamume kabisa, na kila mwanamke ambaye amelala na mwanamume.

1 Samweli 15 : 33
33 Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za BWANA huko Gilgali.

2 Samweli 8 : 2
2 ① Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi.

2 Wafalme 8 : 12
12 ④ Hazaeli akasema, Bwana wangu analilia nini? Akajibu, Kwa sababu nayajua mabaya utakayowatenda wana wa Israeli; utazichoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, utawasetaseta watoto wao wachanga na wanawake wao wenye mimba utawapasua.

Yeremia 39 : 6
6 Ndipo mfalme wa Babeli akawaua wana wa Sedekia huko Ribla mbele ya macho yake; pia mfalme wa Babeli akawaua wakuu wote wa Yuda.

2 Mambo ya Nyakati 25 : 12
12 Na elfu kumi wengine, ambao wana wa Yuda waliwachukua wakiwa hai, wakawaleta juu ya jabali, wakawaangusha chini toka juu ya jabali, hadi wakavunjikavunjika wote.

2 Wafalme 8 : 12
12 ④ Hazaeli akasema, Bwana wangu analilia nini? Akajibu, Kwa sababu nayajua mabaya utakayowatenda wana wa Israeli; utazichoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, utawasetaseta watoto wao wachanga na wanawake wao wenye mimba utawapasua.

2 Wafalme 15 : 16
16 Ndipo Menahemu akapiga Tifsa, na wote waliokuwamo, na mipaka yake, toka Tirza; kwa sababu hawakumfungulia, kwa hiyo akaupiga; nao wanawake wote waliokuwamo wenye mimba akawapasua.

Amosi 1 : 13
13 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao;

2 Samweli 12 : 31
31 Naye akawatoa watu waliokuwamo, akawaweka kwenye kazi ya[10] misumeno, na sululu za chuma, na mashoka ya chuma, akawafanyiza kazi tanurini mwa matofali; ndivyo alivyoifanya miji yote ya wana wa Amoni. Kisha Daudi akarudi na watu wote Yerusalemu.

1 Mambo ya Nyakati 20 : 3
3 Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawawafanyisha kazi kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote.

Waamuzi 16 : 21
21 Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.

Yeremia 39 : 7
7 Pamoja na hayo akampofusha macho Sedekia, akamfunga kwa pingu ili amchukue mpaka Babeli.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *