Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Meno
Mithali 10 : 26
26 Kama siki menoni, na kama moshi machoni, Ndivyo alivyo mtu mvivu kwa hao waliomwajiri.
Zaburi 112 : 10
10 ⑳ Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuondoka, Matumaini ya wasio haki hupotea.
Maombolezo 2 : 16
16 ⑤ Juu yako adui zako wote Wamepanua vinywa vyao; Huzomea, husaga meno yao, Husema, Tumemmeza; Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia; Tumeipata, tumeiona.
Mathayo 8 : 12
12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Mathayo 13 : 42
42 ⑤ na kuwatupa katika tanuri ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Mathayo 13 : 50
50 na kuwatupa katika tanuri ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Mathayo 22 : 13
13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Mathayo 24 : 51
51 ⑮ atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Mathayo 25 : 30
30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Marko 9 : 18
18 na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze.
Luka 13 : 28
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Abrahamu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.
Leave a Reply