Biblia inasema nini kuhusu Mbuni – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mbuni

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mbuni

Ayubu 39 : 18
18 Wakati anapojiinua juu aende, Humdharau farasi na mwenye kumpanda.

Maombolezo 4 : 3
3 ⑧ Hata mbwamwitu hutoa matiti, Huwanyonyesha watoto wao; Binti ya watu wangu amekuwa mkali, Mfano wa mbuni jangwani.

Isaya 13 : 21
21 ⑩ Lakini huko watalala wanyama wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko.

Isaya 34 : 13
13 Miiba itamea majumbani mwake, upupu na mbigili ndani ya maboma yake; nayo itakuwa kao la mbweha, na ua la mbuni.

Isaya 43 : 20
20 Wanyama pori wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu;

Mika 1 : 8
8 Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia, Nitakwenda nimevua nguo, nikiwa uchi; Nitaomboleza kama mbweha, Na kulia kama mbuni.

Mambo ya Walawi 11 : 16
16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;

Kumbukumbu la Torati 14 : 15
15 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;

Ayubu 30 : 29
29 ⑳ Mimi ni ndugu yao mbwamwitu, Ni mwenzao mbuni.

Isaya 43 : 20
20 Wanyama pori wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu;

Yeremia 50 : 39
39 Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwamwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hakuna mtu atakayekaa huko tangu kizazi hadi kizazi.

Mika 1 : 8
8 Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia, Nitakwenda nimevua nguo, nikiwa uchi; Nitaomboleza kama mbweha, Na kulia kama mbuni.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *