Biblia inasema nini kuhusu mbawa za tai – Mistari yote ya Biblia kuhusu mbawa za tai

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mbawa za tai

Isaya 40 : 31
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Kutoka 19 : 4
4 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi.

Kumbukumbu la Torati 32 : 11
11 Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake; Na kupapatika juu ya makinda yake, Alikunjua mbawa zake, akawatwaa, Akawachukua juu ya mbawa zake;

Isaya 40 : 1 – 31
1 Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu.
2 Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
3 Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
4 Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipoinuka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa;
5 Na utukufu wa BWANA utafunuliwa, Na watu wote[9] watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.
6 Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Watu wote ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la shambani;
7 Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Hakika watu ni majani.
8 Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.
9 Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu.
10 Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na fidia yake i mbele zake.
11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.
12 Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiria mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?
13 Ni nani aliyemwongoza Roho ya BWANA, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake?
14 Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonesha njia ya fahamu?
15 Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana.
16 Lebanoni nao hautoshelezi kwa kuni, wala wanyama wake hawatoshi kwa kafara.
17 Mataifa yote huwa kama si kitu mbele zake; huhesabiwa kwake kuwa duni kabisa na batili.
18 Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani?
19 Sanamu! Fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu huifunika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha.
20 Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi stadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.
21 Je! Hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia?
22 Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;
23 ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia.
24 Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.
25 Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? Asema yeye aliye Mtakatifu.
26 Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.
27 Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, BWANA asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie?
28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka;
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Malaki 4 : 2
2 ⑩ Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *