Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mbakaji
Mwanzo 6 : 11
11 Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.
Mhubiri 4 : 1
1 Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.
Zaburi 72 : 4
4 Na atawatetea watu walioonewa, Awaokoe wahitaji, na kumwaangamiza mdhalimu.
Amosi 5 : 12
12 ⑰ Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.
Zaburi 82 : 3
3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara;
Habakuki 1 : 3
3 Mbona wanionesha uovu, na kunifanya nione mabaya? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea.
Isaya 10 : 1 – 2
1 Ole wao wawekao amri zisizo za haki, na waandishi waandikao sheria za kudhulumu;
2 ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake, na kuwanyang’anya maskini wa watu wangu haki yao; ili wajane wawe mateka yao, na kuwafanya yatima waliofiwa na baba zao kuwa mawindo yao!
Isaya 58 : 6
6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
Zaburi 55 : 23
23 Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Kumbukumbu la Torati 22 : 28 – 29
28 Mtu mume akimwona binti aliye mwanamwali ambaye hajaposwa, akamshika na kulala naye, wakaonekana;
29 yule mwanamume aliyelala naye na ampe baba yake yule binti shekeli hamsini za fedha, kisha na awe mkewe, kwa kuwa amemtweza; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote.
Leave a Reply