Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Marafiki
Yohana 15 : 15
15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Mwanzo 40 : 23
23 Lakini huyo mkuu wa wanyweshaji hakumkumbuka Yusufu, alimsahau.
Waamuzi 19 : 2
2 Kisha huyo suria wake akamkasirikia,[18] akamwacha kwenda nyumbani kwa baba yake huko Bethlehemu-yuda, akakaa huko muda wa miezi minne.
1 Wafalme 2 : 6
6 ⑦ Kwa hiyo ufanye kama ilivyo hekima yako, wala usimwachie mvi zake kushukia Ahera kwa amani.
2 Samweli 15 : 12
12 ⑭ Absalomu alipokuwa akitoa dhabihu alituma Ahithofeli Mgiloni, Mshauri wake Daudi, aitwe kutoka mji wake, yaani, Gilo. Njama zao zikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu walizidi kuongezeka.
Zaburi 35 : 16
16 Bila heshima walinidhihaki kupindukia, Wakanisagia meno yao.
Zaburi 41 : 9
9 Hata rafiki yangu mwandani niliyemtumaini, Aliyekula pamoja nami, Ameniinulia kisigino chake.
Zaburi 55 : 14
14 Tumehusiana vizuri; na kutembea Nyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.
Zaburi 55 : 21
21 Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.
Zaburi 88 : 8
8 Wanijuao umewatenga nami; Umenifanya kuwa chukizo kwao; Nimefungwa wala siwezi kutoka.
Zaburi 88 : 18
18 Mpenzi na rafiki umewatenga nami, Nao wanijuao wamo gizani.
Mathayo 26 : 49
49 Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu.
Mathayo 26 : 56
56 Lakini haya yote yamekuwa, ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
Leave a Reply