Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mafanikio
Mwanzo 33 : 11
11 Tafadhali pokea zawadi yangu iliyoletwa kwako, kwa sababu Mungu amenineemesha, na kwa sababu ninavyo hivi vyote. Akamsihi sana, naye akapokea.
Mwanzo 49 : 26
26 Baraka za baba yako Ni nyingi kuliko za milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake, yeye aliyeteuliwa kati ya ndugu zake.
Zaburi 127 : 1
1 BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure.
Zaburi 128 : 2
2 Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.
Mhubiri 7 : 14
14 Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lolote litakalofuata baada yake.
Kumbukumbu la Torati 8 : 18
18 ⑳ Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Kumbukumbu la Torati 31 : 20
20 ⑳ Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu.
Kumbukumbu la Torati 32 : 15
15 Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
Yeremia 5 : 7
7 ⑰ Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba.
Hosea 13 : 6
6 Kwa kadiri ya malisho yao, kwa kadiri iyo hiyo walishiba; walishiba na moyo wao ukatukuka; ndiyo sababu wamenisahau mimi.
Hosea 4 : 7
7 Kadiri walivyozidishwa, kwa kadiri iyo hiyo walinitenda dhambi; nami nitageuza utukufu wao kuwa aibu.
2 Mambo ya Nyakati 32 : 25
25 Walakini Hezekia hakuwa na shukrani kadiri alivyofadhiliwa; kwa kuwa moyo wake ulijawa na kiburi; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu.
2 Mambo ya Nyakati 12 : 1
1 Ikawa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliiacha Torati ya BWANA, na Israeli wote pamoja naye.
2 Mambo ya Nyakati 26 : 16
16 ⑤ Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi BWANA, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa BWANA, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
Ayubu 12 : 5
5 Katika mawazo yake huyo aliye na raha mna kudharau balaa; Tayari kwa ajili ya wenye kuteleza miguu.
Leave a Reply