Biblia inasema nini kuhusu mababu – Mistari yote ya Biblia kuhusu mababu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mababu

Mithali 17 : 6
6 Wana wa wana ndio taji la wazee, Na utukufu wa watoto ni baba zao.

Mithali 16 : 31
31 Kichwa chenye mvi ni taji la utukufu, Kama kikionekana katika njia ya haki.

Zaburi 145 : 4
4 Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu.

Tito 2 : 1 – 5
1 Lakini wewe, nena mambo yanayoambatana na mafundisho mema;
2 ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika subira.
3 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wanaofundisha yaliyo mema;
4 ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;
5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.

Kumbukumbu la Torati 4 : 9
9 ⑩ Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;

Mithali 13 : 22
22 ⑳ Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.

Isaya 46 : 4
4 na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.

2 Timotheo 1 : 5
5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika nyanya yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.

Zaburi 103 : 17
17 ⑫ Bali fadhili za BWANA ni kwa wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ni kwa vizazi vyote;

Zaburi 90 : 12
12 ⑯ Basi, utufundishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.

Kutoka 34 : 6 – 7
6 ⑧ BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
7 ⑩ mwenye kuwaonea huruma watu maelfu,[36] mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.

Zaburi 92 : 14 – 15
14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.
15 Watangaze ya kuwa BWANA ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.

Zaburi 37 : 25
25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula.

Mithali 17 : 22
22 Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.

Isaya 40 : 28 – 31
28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka;
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *