Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kwenda kanisani
Waraka kwa Waebrania 10 : 24 โ 25
24 โช tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;
25 โซ wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Zaburi 150 : 1 โ 6
1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.
2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 โ Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.
Wakolosai 3 : 16
16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
1 Timotheo 3 : 14 โ 15
14 Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu.
15 โฉ Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
Zaburi 122 : 1 โ 9
1 Nilifurahi waliponiambia, Twende nyumbani kwa BWANA.
2 Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
3 Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana,
4 Huko ndiko wapandako kabila, makabila ya BWANA; Kama ulivyowaamuru Waisraeli, Walishukuru jina la BWANA.
5 Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya ukoo wa Daudi.
6 Uombeeni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao;
7 Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe.
9 Kwa ajili ya nyumba ya BWANA, Mungu wetu, Nitakuombea mema.
2 Timotheo 2 : 15
15 Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.
Matendo 2 : 47
47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Mathayo 6 : 5
5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
Leave a Reply