Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuwachukia wazazi wako
Luka 14 : 26
26 ⑥ Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wa kiume na wa kike; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. ⑦
Kumbukumbu la Torati 27 : 16
16 ⑧ Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
Kutoka 20 : 5
5 ⑰ Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Ufunuo 21 : 8
8 ⑥ Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Leave a Reply