Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuwa kimya
Mithali 17 : 28
28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
Yakobo 1 : 19
19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Mithali 11 : 12
12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
Kutoka 14 : 14
14 ⑦ BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Zaburi 4 : 4
4 Muwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
Mithali 29 : 11
11 Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
Ayubu 6 : 24
24 ⑲ Nifunzeni, nami nitanyamaa kimya; Mkanijulishe ni jambo gani nililokosa.
Mithali 10 : 8
8 Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.
1 Wathesalonike 4 : 11 – 12
11 ⑰ Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;
12 ⑱ ili mwende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu chochote.
1 Petro 3 : 3 – 4
3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
Mithali 18 : 13
13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.
Maombolezo 3 : 26
26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu.
Yakobo 3 : 1 – 18
1 ⑫ Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.
2 ⑬ Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.
3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili watutii, hivi twageuza mwili wao wote.
4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, kokote anakoazimia kwenda nahodha.
5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivunia matendo makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6 ⑭ Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.
7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.
8 ⑮ Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9 ⑯ Kwa huo tunamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo unwawalaani wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.
13 ⑰ Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aoneshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
14 ⑱ Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.
15 ⑲ Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya kidunia, ya tabia ya kibinadamu, na ya kishetani.
16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.
17 ⑳ Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
18 Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
Zaburi 46 : 10
10 ⑰ Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
Zaburi 37 : 7
7 Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
Isaya 26 : 3
3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
1 Wafalme 19 : 11 – 12
11 ① Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za BWANA. Na tazama, BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunjavunja miamba mbele za BWANA; lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi;
12 ② na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.
Isaya 30 : 15
15 Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.
Zaburi 35 : 20
20 Maana hawasemi maneno ya amani, Ila juu ya watulivu wa nchi huwaza hila.
Leave a Reply