Biblia inasema nini kuhusu kuvaa kwa ajili ya kanisa – Mistari yote ya Biblia kuhusu kuvaa kwa ajili ya kanisa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuvaa kwa ajili ya kanisa

1 Samweli 16 : 7
7 Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

Kumbukumbu la Torati 22 : 5
5 ⑰ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.

1 Timotheo 2 : 9
9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

1 Wakorintho 6 : 20
20 ⑳ maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Ufunuo 19 : 8
8 ⑱ Naye ameruhusiwa kuvikwa kitani nzuri, ing’aayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

Warumi 14 : 10
10 ⑰ Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.

Tito 3 : 9
9 ④ Lakini ujiepushe na mabishano ya kipumbavu, nasaba, magomvi, na mabishano ya sheria. Kwa kuwa hayana manufaa, tena hayafai kitu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *