Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kutokuwa na shukrani
Hesabu 11 : 4 – 6
4 Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, Ni nani atakayetupa nyama tule?
5 Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu;
6 lakini sasa roho zetu zimekauka; hakuna kitu chochote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu.
1 Yohana 2 : 16
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Leave a Reply