Biblia inasema nini kuhusu kutia moyo – Mistari yote ya Biblia kuhusu kutia moyo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kutia moyo

Yoshua 1 : 9
9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.

2 Timotheo 1 : 7
7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Zaburi 37 : 4
4 Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako.

Zaburi 121 : 1 – 8
1 Nayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu hutoka kwa BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.
3 Hatauacha mguu wako usogezwe; Akulindaye hatasinzia;
4 Naam, hatasinzia wala hatalala, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia.
6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
7 BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

Mithali 30 : 5
5 ⑲ Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.

Zaburi 28 : 7
7 ④ BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.

Zaburi 34 : 4
4 ② Nilimtafuta BWANA, naye akanijibu, Akaniokoa kutoka kwa hofu zangu zote.

Marko 11 : 24
24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

Wafilipi 4 : 13
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

1 Wathesalonike 5 : 9 – 11
9 Kwa kuwa Mungu hakutuweka ili tupate hasira yake, bali ili tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;
10 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tunakesha au tunalala.
11 Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, hakika kama mnavyofanya.

Yeremia 29 : 11
11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.

Zaburi 126 : 5
5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.

Waraka kwa Waebrania 4 : 12
12 ⑳ Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Warumi 15 : 13
13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Zaburi 55 : 22
22 Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.

Waraka kwa Waebrania 10 : 25
25 ⑫ wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Yeremia 29 : 11 – 14
11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.
12 ⑥ Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
13 ⑦ Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
14 ⑧ Nami nitaonekana kwenu, asema BWANA, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema BWANA; nami nitawaleta tena, hadi mahali ambapo kutoka hapo niliwafanya mchukuliwe mateka.

Warumi 15 : 4
4 Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.

2 Wathesalonike 2 : 16 – 17
16 Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,
17 awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.

1 Timotheo 4 : 1 – 168

1 ⑫ Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 ⑬ wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 ⑭ Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
6 Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoefu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.
7 ⑮ Bali hadithi za kale, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.
8 ⑯ Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
9 ⑰ Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa;
10 ⑱ kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa wale waaminio.
11 Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.
12 ⑲ Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
13 Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma Maandiko, kuonya na kufundisha.
14 ⑳ Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
15 Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.
16 Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako, na wale wakusikiao pia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *