Biblia inasema nini kuhusu Kusulubishwa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kusulubishwa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kusulubishwa

Wagalatia 3 : 13
13 ⑩ Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

Mathayo 27 : 38
38 ⑥ Wakati uo huo wanyang’anyi wawili wakasulubiwa pamoja naye, mmoja katika mkono wake wa kulia, na mmoja katika mkono wake wa kushoto.

Warumi 6 : 6
6 mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;

Wagalatia 2 : 20
20 ① Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

Wagalatia 5 : 24
24 ⑰ Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *