Biblia inasema nini kuhusu kusaidia – Mistari yote ya Biblia kuhusu kusaidia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kusaidia

1 Yohana 1 : 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.

Kumbukumbu la Torati 22 : 4
4 Umwonapo punda wa nduguyo, au ng’ombe wake, ameanguka kando ya njia, usijifiche kama usiyemwona; sharti umsaidie kumwinua tena.

Luka 12 : 33
33 ④ Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwizi, wala nondo haharibu. ⑤

Yakobo 1 : 27
27 Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

Luka 16 : 19 – 31
19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa walikuwa wakija na kumramba vidonda vyake.
22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Abrahamu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Abrahamu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
24 Akalia, akasema, Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
25 Abrahamu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo yako mema katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unateseka.
26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
29 Abrahamu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
30 Akasema, La, baba Abrahamu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishika hata mtu akifufuka katika wafu.

Mathayo 25 : 35 – 36
35 kwa maana nilikuwa na njaa, mkanipa chakula; nilikuwa na kiu, mkaninywesha; nilikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nilikuwa uchi, mkanivika nilikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nilikuwa kifungoni, mkanijia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *