Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kumshukuru Mungu
1 Wathesalonike 5 : 18
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Waefeso 5 : 20
20 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Zaburi 136 : 26
26 Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Zaburi 103 : 2
2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote.
Zaburi 106 : 1 – 2
1 Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA, Au kuzihubiri sifa zake zote?
Mathayo 6 : 33
33 ⑩ Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Yohana 3 : 16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
2 Petro 3 : 9
9 ⑯ Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba.
Mathayo 7 : 7
7 ⑮ Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
Warumi 12 : 1 – 21
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;
5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa ni unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;
7 ikiwa ni huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;
8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; msimamizi, na asimamie kwa bidii; anayerehemu, na arehemu kwa furaha.
9 Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkilishika lililo jema.
10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
11 kwa bidii, bila kulegea; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali;
13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.
14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.
16 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.
17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
18 Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Zaburi 100 : 4
4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
Wafilipi 4 : 13
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Zaburi 23 : 1 – 6
1 BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
1 Petro 2 : 21
21 ⑱ Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
Yohana 6 : 11
11 Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka.
Wagalatia 5 : 22
22 ⑮ Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
Mathayo 16 : 24
24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Mithali 16 : 18
18 Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
Isaya 53 : 1 – 12
1 Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani?
2 Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani angeyajali? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
9 ① Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
10 ② Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
11 ③ Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
12 ④ Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawana nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.
Leave a Reply