Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kukata nywele
1 Wakorintho 11 : 6
6 Maana mwanamke asipojifunika kichwa, na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunike kichwa.
Mambo ya Walawi 19 : 27
27 Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.
1 Wakorintho 11 : 13 – 16
13 Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunika kichwa?
14 Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?
15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.
16 Lakini mtu yeyote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.
Ezekieli 44 : 20
20 Hawatanyoa vichwa vyao, wala hawataacha nywele zao kuwa ndefu sana; watazipunguza nywele za vichwa vyao tu.
1 Wakorintho 11 : 14
14 Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?
Mambo ya Walawi 19 : 28
28 Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.
1 Timotheo 2 : 9 – 10
9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
Hesabu 6 : 5
5 Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimguse kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa BWANA, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu.
Mambo ya Walawi 21 : 5
5 ⑯ Wasijifanyie upara kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje tojo katika miili yao.
Mathayo 10 : 30
30 lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.
Leave a Reply