Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kujitambua
Warumi 12 : 3
3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
1 Timotheo 4 : 16
16 Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako, na wale wakusikiao pia.
2 Petro 1 : 3
3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
Wagalatia 6 : 3
3 Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.
Maombolezo 3 : 37 – 40
37 Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza?
38 Je! Katika kinywa chake Aliye Juu Hayatoki maovu na mema?
39 Mbona anung’unika mwanadamu aliye hai Mtu akiadhibiwa kwa dhambi zake?
40 Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, Na kumrudia BWANA tena.
Mathayo 11 : 28 – 30
28 Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
2 Wakorintho 13 : 5
5 ② Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.
1 Wakorintho 13 : 12
12 Maana sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.
Yeremia 17 : 9
9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Mathayo 16 : 24 – 25
24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
Mithali 21 : 2
2 ⑮ Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo.
Mithali 14 : 8
8 Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
Zaburi 8 : 1 – 9
1 Ee, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
2 ⑯ Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mjilipiza kisasi.
3 ⑰ Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;
4 ⑱ Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?
5 Umemfanya mdogo kuliko Mungu; Umemvika taji la utukufu na heshima;
6 ⑲ Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7 Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa porini;
8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
9 ⑳ Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!
Leave a Reply