Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kujisifu
Mithali 20 : 14
14 Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu.
Mithali 25 : 14
14 ⑮ Kama mawingu na upepo pasipo mvua; Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo.
Mithali 27 : 1
1 Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.
Isaya 10 : 15
15 ⑱ Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.
Yeremia 9 : 23
23 ⑯ BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;
Warumi 1 : 30
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
Yakobo 3 : 5
5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivunia matendo makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
Yakobo 4 : 16
16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya.
Zaburi 52 : 1
1 ⑧ Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.
1 Wafalme 20 : 10
10 ⑬ Ndipo Ben-hadadi akatuma kwake, akasema, Miungu wanifanyie hivi na kuzidi, yakiwa mavumbi ya Samaria yatatosha makonzi ya watu wote walio miguuni pangu.
2 Wafalme 18 : 19
19 ⑩ Yule amiri[12] akawaambia, Haya, mwambieni Hezekia, kusema, Mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, asema hivi, Ni tumaini gani hili unalolitumainia?
Isaya 10 : 15
15 ⑱ Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.
Luka 10 : 17
17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.
Luka 10 : 20
20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.
Zaburi 49 : 9
9 ndipo aishi milele asilione kaburi.
Zaburi 52 : 1
1 ⑧ Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.
Zaburi 94 : 4
4 Je! Wote watendao uovu watatoa maneno, Na kusema majivuno, na kufanya kiburi?
Warumi 3 : 31
31 Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? La hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.
Warumi 11 : 21
21 Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.
1 Wakorintho 1 : 31
31 kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.
1 Wakorintho 4 : 7
7 Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?
2 Wakorintho 10 : 17
17 ⑦ Lakini, Yeye ajisifuye, na ajisifu katika Bwana.
Waefeso 2 : 10
10 ⑤ Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Leave a Reply