Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kujipendekeza
Ayubu 17 : 5
5 Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo, Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.
Ayubu 32 : 22
22 Kwa kuwa mimi sijui kujipendekeza; Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.
Zaburi 5 : 9
9 Maana vinywani mwao hamna uaminifu; Moyo wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, Ulimi wao hujipendekeza.
Zaburi 12 : 3
3 BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Na ulimi unenao maneno ya kiburi;
Zaburi 36 : 2
2 Kwa maana hujipendekeza machoni pake Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.
Zaburi 49 : 13
13 Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao, Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao.
Zaburi 49 : 18
18 Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai, Na watu watakusifu ukijitendea mema,
Mithali 6 : 24
24 Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.
Zaburi 78 : 36
36 Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, Wakamwambia uongo kwa ndimi zao.
Mithali 5 : 3
3 Maana midomo ya malaya hudondosha asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
Mithali 7 : 5
5 Wapate kukulinda na malaya, Na mwasherati akubembelezaye kwa maneno yake.
Mithali 7 : 21
21 Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
Mithali 14 : 20
20 Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana marafiki wengi.
Mithali 19 : 4
4 Utajiri huongeza marafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake.
Mithali 19 : 6
6 Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili; Na kila mtu ni rafiki yake atoaye zawadi.
Mithali 20 : 19
19 Mwenye udaku hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.
Mithali 22 : 16
16 Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara.
Mithali 24 : 24
24 ⑤ Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Makabila ya watu watamlaani, taifa watamchukia.
Mithali 25 : 26
26 Mwenye haki amwangukiapo mtu mbaya Ni kama chemchemi iliyochafuka, Na kisima kilichokanyagwa.
Mithali 26 : 28
28 Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.
Mithali 27 : 21
21 Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake.
Mithali 28 : 23
23 Amkemeaye mwenzake hatimaye atapata kibali; Zaidi ya mtu ajipendekezaye kwa ulimi wake.
Mithali 29 : 5
5 Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.
Danieli 11 : 21
21 Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.
Danieli 11 : 34
34 Basi watakapoanguka, watasaidiwa kwa msaada kidogo; lakini wengi wataambatana nao kwa maneno ya kujipendekeza.
Luka 6 : 26
26 Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo.
Wagalatia 1 : 10
10 Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
1 Wathesalonike 2 : 1 – 232
1 Maana ninyi wenyewe, ndugu, mnakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure;
2 ingawa tuliteswa na kutukanwa, katika Filipi kama mjuavyo, tulithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.
3 Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila;
4 bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.
5 Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wowote, kama mjuavyo, wala maneno ya juu juu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.
6 Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine, ingawa tungeweza kuwalemea kama Mitume wa Kristo;
7 bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.
8 Hivyo ndivyo nasi tukiwajali kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.
9 Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, huku tukiwahubiria Injili ya Mungu.
10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;
11 vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia;
12 ili mwende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.
13 Kwa sababu hiyo sisi nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe wa Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na kwa kweli ndivyo lilivyo; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.
14 Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yudea, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi;
15 ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wowote;
16 huku wakituzuia tusiseme na Mataifa wapate kuokolewa; ili watimize dhambi zao siku zote. Lakini hasira imewafikia hata mwisho.
17 Lakini sisi, ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa muda, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu.
18 Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, nilitaka kuja mara kwa mara, lakini Shetani akatuzuia.
19 Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji la kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?
20 Maana ninyi ndinyi utukufu wetu, na furaha yetu.
Leave a Reply