Biblia inasema nini kuhusu Kuchonga – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kuchonga

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kuchonga

Kutoka 32 : 4
4 ⑫ Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.

Kutoka 28 : 11
11 Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile mihuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.

Kutoka 28 : 21
21 Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa mihuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hayo makabila kumi na mawili.

Kutoka 28 : 36
36 Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa michoro ya mihuri, MTAKATIFU KWA BWANA.

Kutoka 39 : 14
14 Na hivyo vito vilikuwa vyaandama majina ya wana wa Israeli, kumi na mawili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora mihuri, kila moja kwa jina lake, kwa yale makabila kumi na mawili.

Kutoka 39 : 6
6 ⑧ Nao wakavitengeza vile vito vya shohamu, vilivyotiwa katika vijalizo vya dhahabu, vilivyochorwa mfano wa kuchora kwake mhuri, kwa majina ya hao wana wa Israeli.

Kutoka 39 : 30
30 ⑲ Nao wakafanya hilo bamba la hilo taji takatifu la dhahabu safi, na kuandika juu yake andiko, mfano wa kuchorwa kwa mhuri, MTAKATIFU KWA BWANA.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *