Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kucheza
Kutoka 15 : 20
20 Na Miriamu, nabii mwanamke, dada yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.
Kutoka 32 : 19
19 Hata alipokaribia kambini akaiona ile ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.
Waamuzi 11 : 34
34 ⑦ Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na akichezacheza; naye alikuwa ni mwanawe wa pekee; hakuwa na mwingine, wa kiume wala binti.
Waamuzi 21 : 21
21 ⑧ kaeni macho; kisha tazameni, kisha hao binti za Shilo watakapotoka ili wacheze katika hiyo michezo, basi tokeni mizabibuni, na kila mtu na ajishikie mke katika hao binti za Shilo, kisha mrudi katika nchi ya Benyamini.
1 Samweli 18 : 6
6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda.
1 Samweli 21 : 11
11 Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, Je! Huyu siye yule Daudi, mfalme wa nchi? Je! Hawakuimbiana habari zake katika ngoma zao, kusema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.
1 Samweli 30 : 16
16 Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.
2 Samweli 6 : 16
16 Ikawa, sanduku la BWANA lilipoingia mji wa Daudi, Mikali binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele za BWANA; akamdharau moyoni mwake.
Ayubu 21 : 11
11 Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza.
Zaburi 30 : 11
11 ⑱ Umegeuza msiba wangu kuwa ngoma; Umeniondolea huzuni yangu, kunijalia furaha tele.
Zaburi 149 : 3
3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa sauti tamu ya matari na kinubi.
Zaburi 150 : 4
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
Mhubiri 3 : 4
4 ⑦ Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
Yeremia 31 : 4
4 Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi.
Yeremia 31 : 13
13 Ndipo bikira atafurahi katika kucheza, na vijana na wazee pamoja; maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha, nami nitawafariji, na kuwafurahisha waache huzuni zao.
Maombolezo 5 : 15
15 Furaha ya mioyo yetu imekoma; Machezo yetu yamegeuka maombolezo.
Mathayo 11 : 17
17 Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.
Luka 15 : 25
25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwa shambani na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na nderemo.
Mathayo 14 : 6
6 Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.
Marko 6 : 22
22 ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lolote utakalo, nitakupa.
Kutoka 32 : 19
19 Hata alipokaribia kambini akaiona ile ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.
Kutoka 32 : 25
25 Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, na kuwa dhihaka kati ya adui zao,
Leave a Reply