Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kinubi
Isaya 38 : 20
20 BWANA yu tayari kunipa wokovu. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.
Ezekieli 33 : 32
32 Na tazama, wewe umekuwa kwao kama wimbo mzuri sana, wa mtu mwenye sauti ipendezayo, awezaye kupiga kinanda vizuri; maana, wasikia maneno yako, lakini hawayatendi.
Habakuki 3 : 19
19 MUNGU, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.[3]
1 Samweli 18 : 6
6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda.
Zaburi 33 : 2
2 Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
Zaburi 92 : 3
3 Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi.
Zaburi 144 : 9
9 ⑥ Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.
Zaburi 150 : 4
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
Mwanzo 4 : 21
21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba ya wote wapigao kinubi na filimbi.
1 Wafalme 10 : 12
12 Mfalme akafanya kwa miti hiyo ya msandali nguzo za nyumba ya BWANA, na za nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda vya hao waimbaji; wala haikuja miti ya msandali kama hiyo, wala haikuonekana, hata leo.
1 Samweli 16 : 16
16 Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona.
1 Samweli 16 : 23
23 Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli, ndipo Daudi alipokishika kinubi na kukipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.
1 Samweli 10 : 5
5 ⑦ Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri;
1 Mambo ya Nyakati 16 : 5
5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Metithia, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;
1 Mambo ya Nyakati 25 : 7
7 ⑦ Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia BWANA, wote waliokuwa mastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane.
2 Mambo ya Nyakati 5 : 13
13 hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA,
2 Mambo ya Nyakati 29 : 25
25 ⑪ Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa BWANA wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani BWANA aliamuru hivi kwa manabii wake.
Zaburi 33 : 2
2 Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
Zaburi 43 : 4
4 Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.
Zaburi 49 : 4
4 Nitatega sikio langu nisikie mithali, Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi.
Zaburi 57 : 8
8 Amka, ee moyo wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.
Zaburi 71 : 1 – 232
1 Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele.
2 Kwa haki yako uniponye, uniponye, Unitegee sikio lako, uniokoe.
3 ② Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Ngome imara ya wokovu wangu. Maana wewe, Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.
4 Ee Mungu wangu, uniponye mkononi mwa mkorofi, Katika mkono wake mwovu na mdhalimu,
5 ③ Maana ndiwe tegemeo langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.
6 ④ Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.
7 ⑤ Nimekuwa kifani kwa watu wengi, Lakini wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.
8 Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa.
9 Usinitupe wakati wa uzee, Nguvu zangu zipungukapo usiniache.
10 ⑥ Kwa maana adui zangu wananiamba, Nao wanaotaka kuniua hushauriana.
11 Wakisema, Mungu amemwacha, Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya.
12 ⑦ Ee Mungu, usiwe mbali nami; Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia.
13 ⑧ Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.
14 Lakini mimi nitakutumainia daima, Nitaendelea kukusifu zaidi na zaidi.
15 ⑩ Lakini mimi nitakutumainia daima Na nitaendelea kukusifu zaidi na zaidi.
16 ⑪ Nitakuja na mambo ya ajabu ya Bwana MUNGU; Nitawakumbusha watu haki yako Wewe peke yako.
17 Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.
18 Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
19 ⑫ Na haki yako, Ee Mungu, Imefika juu sana. Wewe uliyefanya mambo makuu; Ee Mungu, ni nani aliye kama Wewe?
20 ⑬ Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Kutoka katika vina virefu chini ya nchi.
21 Laiti ungeniongezea ukuu! Urejee tena na kunifariji moyo.
22 ⑭ Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli.
23 ⑮ Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo, Na nafsi yangu uliyoikomboa.
24 Ulimi wangu nao utasimulia Haki yako mchana kutwa. Kwa maana wameaibishwa, Wametahayarika, wanaonitakia mabaya.
Leave a Reply