Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kikapu
Mwanzo 40 : 17
17 Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu.
Kutoka 29 : 3
3 Nawe vitie vyote katika kikapu, uvilete ndani ya kikapu, pamoja na huyo ng’ombe, na hao kondoo dume wawili.
Kutoka 29 : 23
23 ⑦ utwae na mkate mmoja wa unga, na mkate mmoja ulioandaliwakwa mafuta, na kaki moja katika kile kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, kilichowekwa mbele ya BWANA;
Kutoka 29 : 32
32 ⑯ Na Haruni na wanawe wataila ile nyama ya kondoo, na mikate iliyo katika kile kikapu, hapo mbele ya mlango wa hema ya kukutania.
Mambo ya Walawi 8 : 2
2 Mtwae Haruni, na wanawe pamoja naye, na yale mavazi, na mafuta ya kutia, na ng’ombe dume wa sadaka ya dhambi, na kondoo wawili wa kiume, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu;
Hesabu 6 : 15
15 ⑤ na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, mikate ya unga mwembamba iliyokandwa kwa mafuta, na mikate ya kaki isiyochachwa, iliyotiwa mafuta, pamoja na sadaka zake za unga, na sadaka zake za kinywaji.
Kumbukumbu la Torati 26 : 2
2 twaa malimbuko ya ardhi, utakayoyavuna katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako; ukayatie katika kikapu, ukaende hata mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wako, ili alikalishe jina lake huko.
Kumbukumbu la Torati 28 : 5
5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
Kumbukumbu la Torati 28 : 17
17 Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.
2 Wafalme 10 : 7
7 Ikawa, barua ilipowawasilia, waliwatwaa hao wana wa mfalme, wakawaua, watu sabini, wakatia vichwa vyao katika makapu, wakampelekea huko Yezreeli.
Mathayo 14 : 20
20 Wakala wote wakashiba; wakayaokota mabaki ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.
Mathayo 15 : 37
37 Wakala wote wakashiba; wakayaokota mabaki ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.
Mathayo 16 : 10
10 ⑩ Wala ile mikate saba kwa watu elfu nne, na makanda mangapi mliyoyaokota?
Matendo 9 : 25
25 Wanafunzi wake wakamtwaa usiku wakamshusha ukutani, wakimteremsha katika kapu.
2 Wakorintho 11 : 33
33 nami nikateremshwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka katika mikono yake.
Leave a Reply