Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kapteni
Kumbukumbu la Torati 20 : 9
9 Itakuwa hapo watakapokwisha wale makamanda kusema na watu, na waweke majemadari wa majeshi juu ya watu.
Waamuzi 4 : 2
2 BWANA akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa kamanda wa jeshi lake.
1 Samweli 14 : 50
50 na jina lake mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu, binti Ahimaasi. Tena, jina la jemadari wa jeshi lake aliitwa Abneri, mwana wa Neri, aliyekuwa baba mdogo wa Sauli.
1 Wafalme 2 : 35
35 Kisha mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yehoyada, mahali pake juu ya jeshi; na Sadoki, kuhani, mfalme akamweka mahali pa Abiathari.
1 Wafalme 16 : 16
16 Na hao watu waliokuwako kambini wakasikia habari ya kwamba Zimri amekula njama, tena amemwua mfalme; kwa hiyo Israeli wote wakamfanya Omri, jemadari wa jeshi, awe mfalme juu ya Israeli siku ile kambini.
1 Mambo ya Nyakati 27 : 34
34 na, baada ya Ahithofeli, walikuwa Yehoyada mwana wa Benaya, na Abiathari; na jemadari wa jeshi la mfalme alikuwa Yoabu.
Hesabu 31 : 48
48 Na majemadari waliokuwa juu ya maelfu ya hilo jeshi, na viongozi wa maelfu, na viongozi wa mamia, wakamkaribia Musa;
1 Samweli 17 : 18
18 ② mpelekee kamanda wa kikosi chao jibini hizi kumi, ukawaangalie, wako hali gani, kisha uniletee jawabu yao.
1 Mambo ya Nyakati 28 : 1
1 Kisha Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli, wakuu wa kabila, na makamanda wa vikosi wenye kumtumikia mfalme kwa zamu, na makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, na wenye kutawala juu ya mali na milki za mfalme, na za wanawe, pamoja na matowashi, na mashujaa, naam, wanaume mashujaa wote.
2 Wafalme 1 : 9
9 Ndipo mfalme akatuma kamanda wa askari hamsini pamoja na hamsini wake, wamwendee Eliya. Akamwendea, na tazama, ameketi juu ya kilima. Akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka.
Isaya 3 : 3
3 jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye stadi, na mganga ajuaye uganga sana.
Mwanzo 37 : 36
36 ⑲ Nao Wamidiani wakamuuza huko Misri, kwa Potifa, mmoja wa maofisa wa Farao, mkuu wa askari walinzi.
2 Wafalme 25 : 8
8 ⑩ Hata mwezi wa tano, siku ya saba ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na tisa wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia Yerusalemu.
Yeremia 37 : 13
13 Naye alipokuwa katika lango la Benyamini, mkuu wa walinzi alikuwapo, jina lake Iriya, mwana wa Shelemia, mwana wa Hanania; akamkamata Yeremia, nabii, akisema, Unakwenda kujiunga na Wakaldayo.
1 Samweli 9 : 16
16 Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikia.
1 Samweli 22 : 2
2 Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walikuwa kama watu mia nne.
2 Wafalme 20 : 5
5 ⑥ Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA.
1 Mambo ya Nyakati 11 : 21
21 ⑭ Katika wale watatu yeye alikuwa mwenye heshima kuliko hao wawili, akawa kamanda wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu.
Leave a Reply