Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kanisa (2)
Kutoka 12 : 3
3 Waambieni mkutano wote, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;
Kutoka 12 : 6
6 Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.
Kutoka 12 : 19
19 ⑤ Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu yeyote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa kama mgeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi.
Kutoka 12 : 47
47 Na wafanye jambo hili mkutano wa Israeli wote.
Kutoka 16 : 2
2 Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung’unikia Musa na Haruni, huko barani;
Kutoka 16 : 10
10 Ilikuwa Haruni aliponena na huo mkutano wote wa wana wa Israeli, wakaangalia upande wa bara, na tazama, utukufu wa BWANA ukaonekana katika hilo wingu.
Kutoka 16 : 22
22 Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa.
Mambo ya Walawi 4 : 13
13 ⑧ Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi bila kukusudia, na jambo lenyewe likayafichamania macho ya huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na BWANA, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia;
Mambo ya Walawi 4 : 15
15 ⑩ Kisha wazee wa mkutano wataweka mikono yao kichwani mwake huyo ng’ombe mbele za BWANA;
Mambo ya Walawi 10 : 17
17 Kwa nini hamkula hiyo sadaka ya dhambi katika mahali patakatifu, kwa kuwa ni takatifu sana, naye amewapa ninyi ili kuuchukua uovu wa mkutano, na kuwafanyia upatanisho mbele za BWANA?
Mambo ya Walawi 24 : 14
14 Mtoe huyo aliyelaani nje ya kambi; na wale wote waliomsikia na waweke mikono yao kichwani mwake, kisha mkutano wote na wamwue kwa kumpiga kwa mawe.
Mathayo 16 : 18
18 ⑯ Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Mathayo 18 : 17
17 ⑥ Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
Matendo 2 : 47
47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
1 Wakorintho 11 : 18
18 ⑫ Kwa maana kwanza mnapokutanika kanisani nasikia kuna migawanyiko kwenu; nami kwa kiasi fulani naamini;
1 Wakorintho 14 : 19
19 lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, kuliko kunena maneno elfu kumi kwa lugha.
1 Wakorintho 14 : 23
23 ① Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?
1 Wakorintho 14 : 28
28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
1 Wakorintho 14 : 34
34 ⑥ Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
1 Wakorintho 15 : 9
9 ⑮ Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu nililiudhi kanisa la Mungu.
Wagalatia 1 : 13
13 Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba nililitesa kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu.
Zaburi 89 : 7
7 Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
Leave a Reply