Biblia inasema nini kuhusu Kanaani – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kanaani

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kanaani

Mwanzo 9 : 18
18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.

Mwanzo 9 : 22
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

Mwanzo 9 : 27
27 ⑥ Mungu amwongezee Yafethi. Na akae katika hema za Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake.

Mwanzo 10 : 6
6 Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.

Mwanzo 10 : 15
15 Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,

1 Mambo ya Nyakati 1 : 8
8 Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.

Mwanzo 11 : 31
31 Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.

Mwanzo 17 : 8
8 ⑫ Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayokaa kama mgeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.

Mwanzo 23 : 2
2 Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.

Kutoka 15 : 17
17 Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Mahali pale ulipojifanyia, Ee BWANA, ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara, BWANA, kwa mikono yako.

Kutoka 15 : 14
14 Makabila ya watu wamesikia, wanatetemeka, Wakazi wa Ufilisti uchungu umewashika.

1 Samweli 13 : 19
19 Basi, hakukuwa mhunzi yeyote katika nchi yote ya Israeli; kwa kuwa Wafilisti walisema, Waebrania wasije wakajitengenezea panga au mikuki;

Mwanzo 40 : 15
15 ⑰ Kwa sababu hakika niliibwa kutoka nchi ya Waebrania, wala hapa sikutenda jambo lolote hata wanitie gerezani.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *