Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kampuni
Mwanzo 19 : 15
15 Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, la sivyo utapotelea katika maangamizi ya mji huu.
Mwanzo 49 : 6
6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng’ombe;
Kutoka 23 : 2
2 Usiwafuate walio wengi kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;
Kutoka 23 : 33
33 ⑬ Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni (mtego) tanzi kwako.
Kutoka 34 : 15
15 ⑰ Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake.
Kumbukumbu la Torati 7 : 4
4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya BWANA juu yenu, naye atakuangamiza upesi.
Yoshua 23 : 13
13 jueni hakika ya kuwa BWANA, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa haya mbele ya macho yenu, bali watakuwa mtego kwenu na tanzi, na mjeledi mbavuni mwenu, na miiba machoni mwenu, hadi mtakapoangamia na kutoka katika nchi hii njema, ambayo BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi.
Mambo ya Walawi 18 : 3
3 Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mlikokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msifuate amri zao hao.
Mambo ya Walawi 20 : 23
23 ⑩ Nanyi msiende kwa kuzifuata desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia.
Hesabu 16 : 26
26 ② Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao chochote, msiangamizwe katika dhambi zao zote.
Hesabu 33 : 55
55 ⑬ Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtawabakiza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa.
Waamuzi 2 : 3
3 ⑤ Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni mtego kwenu.
Kumbukumbu la Torati 12 : 30
30 ujiangalie, usije ukanaswa ukawafuata, wakiisha kuangamizwa mbele yako; wala usije ukauliza habari za miungu yao, ukisema, Mataifa haya waitumikiaje miungu yao? Nami nifanye hivyo.
2 Samweli 23 : 7
7 Mtu atakayeigusa hiyo, Na awe na chuma na mpini wa mkuki, Nao watateketezwa papo hapo kwa moto.
2 Mambo ya Nyakati 19 : 2
2 Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao BWANA? Kwa ajili ya hayo ghadhabu itokayo kwa BWANA i juu yako.
Ezra 9 : 14
14 ② je! Tuzivunje tena amri zako, tukajiunge na watu wanaotenda machukizo hayo, kwa kuoana nao? Je! Usingekasirika nasi hata kutuangamiza kabisa, pasisalie mabaki yoyote, wala mtu wa kuokoka?
Zaburi 1 : 1
1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Zaburi 6 : 8
8 ⑥ Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.
Zaburi 15 : 4
4 Anayedharau waovu Machoni pake, Bali huwaheshimu wamchao BWANA Aliyeapa ingawa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.
Zaburi 26 : 5
5 Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu.
Zaburi 26 : 9
9 Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na wauaji.
Zaburi 28 : 3
3 Usinikokote pamoja na wasio haki, Wala pamoja na watenda maovu. Wawaambiao jirani zao maneno ya amani, Lakini mioyoni mwao mna madhara.
Zaburi 31 : 6
6 Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumainia BWANA.
Zaburi 50 : 18
18 Ulipomwona mwizi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi.
Zaburi 84 : 10
10 Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu kwingineko; Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kuishi katika hema za uovu.
Zaburi 101 : 4
4 Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu, Lililo ovu sitalijua.
Zaburi 101 : 7
7 Hatakaa ndani ya nyumba yangu Mtu atendaye hila. Asemaye uongo hatathibitika Mbele ya macho yangu.
Zaburi 106 : 35
35 Bali walijichanganya na mataifa, Wakajifunza matendo yao.
Leave a Reply