Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Joram
2 Samweli 8 : 10
10 Tou akamtuma Yoramu mwanawe kwa mfalme Daudi ili kumsalimia, na kumpongeza, na kumbariki, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake Yorabu akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba;
1 Mambo ya Nyakati 18 : 10
10 akamtuma mwanawe Hadoramu kwa mfalme Daudi, ili kumsalimia, na kumbarikia, kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou; naye akaleta vyombo vya dhahabu, na fedha, na shaba, vya namna zote.
2 Wafalme 1 : 17
17 Basi akafa, sawasawa na neno la BWANA alilolinena Eliya. Na Yoramu[1] alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana.
2 Wafalme 3 : 1
1 Basi Yoramu[2] mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka kumi na miwili.
2 Wafalme 5 : 27
27 ⑮ Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.
2 Wafalme 6 : 23
23 Basi akawaandalia chakula tele; nao walipokwisha kula na kunywa, akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikosi vya Shamu havikuja tena katika nchi ya Israeli.
2 Wafalme 8 : 29
29 ⑮ Akarudi Yoramu mfalme, auguzwe katika Yezreeli majeraha waliyotia Washami huko Rama alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.
2 Mambo ya Nyakati 22 : 6
6 Akarudi Yezreeli ili aponye majeraha waliyomjeruhi huko Rama, alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia[24] mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda, akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu, katika Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.
2 Wafalme 8 : 5
5 ① Ikawa, alipokuwa katika kumwambia mfalme jinsi alivyomfufua mtu aliyekufa, tazama, huyo mwanamke aliyemfufulia mwanawe, alimlilia mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. Gehazi akasema, Bwana wangu mfalme, huyu ndiye mwanamke, na huyu ndiye mwanawe, ambaye Elisha alimfufua.
2 Wafalme 9 : 26
26 Hakika, jana nimeiona damu ya Nabothi, na damu ya wanawe, asema BWANA; nami nitakulipa katika kiwanja hiki, asema BWANA. Basi sasa mtwae huyu ukamtupe katika kiwanja hicho, sawasawa na neno la BWANA.
Leave a Reply