Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ibleam
Yoshua 17 : 11
11 Tena Manase alikuwa na miji katika Isakari na katika Asheri, nayo ni hii, Beth-sheani na vijiji vyake, Ibleamu na miji yake, wenyeji wa Dori na miji yake, wenyeji wa Endori na miji yake, wenyeji wa Taanaki na miji yake, wenyeji wa Megido na miji yake, na pia theluthi ya Nafathi.
Waamuzi 1 : 27
27 Tena Manase hakuwatoa wenyeji wa Beth-sheani na miji yake, wala hao waliokaa Taanaki na miji yake, wala hao waliokaa Dori na miji yake, wala hao waliokaa Ibleamu na miji yake, wala hao waliokaa Megido na miji yake; lakini hao Wakanaani walikuwa hawakukubali kuiacha nchi hiyo.
2 Wafalme 9 : 27
27 Na Ahazia mfalme wa Yuda alipoona hayo, akakimbia kwa njia ya nyumba ya bustanini. Yehu akamfuatia, akasema, Mpigeni huyu naye katika gari lake; wakampiga hapo penye kupandia Guri, karibu na Ibleamu. Akakimbilia Megido, akafa huko.
Leave a Reply