Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hoshea
Hesabu 13 : 8
8 Katika kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni
Hesabu 13 : 16
16 ⑮ Hayo ndiyo majina ya hao watu waliotumwa na Musa waende kuipeleleza nchi. Na huyo Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita jina lake Yoshua.
Kumbukumbu la Torati 32 : 44
44 Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni.
1 Mambo ya Nyakati 27 : 20
20 wa wana wa Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia, wa nusu kabila la Manase, Yoeli mwana wa Pedaya;
2 Wafalme 15 : 30
30 Na Hoshea mwana wa Ela akamfitinia Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
2 Wafalme 17 : 2
2 Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, ila si kama wafalme wa Israeli waliomtangulia.
2 Wafalme 17 : 3
3 ⑫ Naye Shalmanesa mfalme wa Ashuru akakwea juu yake, Hoshea akawa mtumishi wake, akampa kodi.
2 Wafalme 17 : 4
4 Mfalme wa Ashuru akaona fitina katika huyo Hoshea; kwa maana alikuwa ametuma wajumbe kwa So, mfalme wa Misri, wala hakumletea kodi mfalme wa Ashuru, kama alivyofanya mwaka kwa mwaka; kwa hiyo mfalme wa Ashuru akamfunga, akamtia kifungoni.
2 Wafalme 17 : 6
6 ⑭ Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi.
2 Wafalme 18 : 12
12 ⑤ kwa sababu hawakuitii sauti ya BWANA, Mungu wao, bali waliyavunja maagano yake, mambo yote ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwaamuru, wasikubali kuyasikiliza, wala kuyatenda.
Hosea 10 : 3
3 Yakini sasa watasema, Hatuna mfalme; kwa maana hatumchi BWANA; na mfalme huyu je! Aweza kututendea nini?
Hosea 10 : 7
7 Katika habari za Samaria, mfalme wake amekatiliwa mbali, kama povu usoni pa maji.
Nehemia 10 : 23
23 Hoshea, Hanania, Hashubu;
Leave a Reply