Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hisani
Mithali 10 : 12
12 ⑮ Kuchukiana huleta fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote.
Mithali 17 : 9
9 Afunikaye kosa hutafuta kupendwa; Bali yeye afichuaye siri hutenga rafiki.
Mathayo 5 : 24
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
Mathayo 6 : 15
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Mathayo 7 : 5
5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Luka 6 : 42
42 Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.
Mathayo 18 : 35
35 ⑬ Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.
Luka 17 : 4
4 Na kama akikukosea mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
Yohana 7 : 24
24 Basi msihukumu kwa kuangalia kwa nje tu,[1] bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.
Warumi 14 : 23
23 Lakini aliye na mashaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
1 Wakorintho 4 : 5
5 Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
1 Wakorintho 10 : 33
33 ④ vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.
1 Wakorintho 13 : 13
13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
1 Wakorintho 16 : 14
14 Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.
Wagalatia 6 : 1
1 ⑳ Ndugu zangu, mtu akishikwa katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
Waefeso 4 : 32
32 ⑱ tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Wakolosai 3 : 14
14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
1 Timotheo 1 : 5
5 Lakini lengo la agizo hili ni kuleta upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.
1 Timotheo 4 : 12
12 ⑲ Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
2 Timotheo 2 : 22
22 ④ Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Yakobo 2 : 13
13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
Yakobo 4 : 12
12 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?
1 Petro 3 : 9
9 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.
Leave a Reply