Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Herodia
Mathayo 14 : 3
3 ⑱ Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye.
Mathayo 14 : 6
6 Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.
Marko 6 : 17
17 ⑲ Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo, ndugu yake, kwa kuwa amemwoa;
Marko 6 : 19
19 Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asiweze.
Marko 6 : 22
22 ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lolote utakalo, nitakupa.
Luka 3 : 19
19 ⑤ Lakini mfalme Herode alipokaripiwa na yeye kwa ajili ya Herodia, mke wa nduguye, na maovu yote aliyoyafanya Herode,
Leave a Reply