Biblia inasema nini kuhusu Hemani – Mistari yote ya Biblia kuhusu Hemani

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hemani

1 Wafalme 4 : 31
31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.

1 Mambo ya Nyakati 2 : 6
6 ⑥ Na wana wa Zera; Zabdi, na Ethani, na Hemani, na Kalkoli, na Darda; hao wote ni watano.

1 Mambo ya Nyakati 6 : 33
33 Na hawa ndio waliohudumu pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli;

1 Mambo ya Nyakati 15 : 17
17 ⑯ Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana wa Kishi;

1 Mambo ya Nyakati 15 : 19
19 Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;

1 Mambo ya Nyakati 16 : 41
41 na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;

1 Mambo ya Nyakati 25 : 5
5 ⑥ hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.

1 Mambo ya Nyakati 6 : 33
33 Na hawa ndio waliohudumu pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli;

1 Mambo ya Nyakati 25 : 6
6 Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa BWANA, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.

Zaburi 88 : 1
1 Ee BWANA, Mungu wa wokovu wangu Mchana na usiku nimelia mbele zako.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *