Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hamor
Mwanzo 33 : 19
19 Akainunua sehemu ya nchi, alipopiga hema yake, kwa mkono wa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia moja vya fedha.
Yoshua 24 : 32
32 Na hiyo mifupa ya Yusufu, ambayo wana wa Israeli walikuwa wameileta kutoka Misri, wakaizika huko Shekemu katika ile sehemu ya nchi, Yakobo aliyoinunua kwa wana wa Hamori, babaye Shekemu, kwa vipande mia moja vya fedha; nayo ikawa ni urithi wa wana wa Yusufu.
Waamuzi 9 : 28
28 ⑦ Naye Gaali mwana wa Ebedi akasema, Abimeleki ni nani, na sisi wa Shekemu ni nani, hata tukamtumikie yeye? Je, huyu mwana wa Yerubaali na Zebuli afisa wake hawakuwatumikia watu wa Hamori babaye Shekemu? Basi, kwa nini tumutumikie?
Mwanzo 34 : 26
26 Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka.
Mwanzo 49 : 6
6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng’ombe;
Matendo 7 : 16
16 ⑮ wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Abrahamu alilinunua kwa kima fulani cha fedha kutoka kwa wana wa Hamori, huko Shekemu.
Leave a Reply