Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Afisa, Civil
Kumbukumbu la Torati 1 : 16
16 Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu, nikawaambia, Sikilizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye.
2 Samweli 8 : 18
18 ⑧ na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi wakawa makuhani.
2 Samweli 20 : 26
26 Tena na Ira, Myairi, alikuwa kuhani kwa Daudi.
1 Wafalme 4 : 19
19 ⑮ Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, na Ogu mfalme wa Bashani; naye alikuwa mkuu pekee katika nchi hiyo.
1 Wafalme 9 : 22
22 Lakini kwa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu yeyote shokoa; ila wao walikuwa askari, watumishi wake, makamanda wake, maafisa wake, makamanda wa magari yake na wapanda farasi wake.
Leave a Reply