Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Goliathi
1 Samweli 21 : 9
9 Yule kuhani akasema, Upanga wa Goliathi, yule Mfilisti, uliyemwua katika bonde la Ela, tazama, upo hapa, umefungwa ndani ya nguo nyuma ya naivera; ukipenda kuuchukua, haya! Uchukue, maana hapa hapana mwingine ila huo tu. Daudi akasema, Hapana mwingine kama ule; haya! Nipe.
1 Samweli 22 : 10
10 Naye akamwuliza BWANA kwa ajili yake, akampa vyakula, akampa na ule upanga wa Goliathi, Mfilisti.
2 Samweli 21 : 22
22 Hao wanne walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi; wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mikono ya watumishi wake.
1 Mambo ya Nyakati 20 : 8
8 Hao walizaliwa kwake huyo Mrefai[18] wa Gathi, nao wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mkono wa watumishi wake.
Leave a Reply