Biblia inasema nini kuhusu ghadhabu ya Mungu – Mistari yote ya Biblia kuhusu ghadhabu ya Mungu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ghadhabu ya Mungu

Warumi 1 : 18
18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.

Yohana 3 : 36
36 ⑩ Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Warumi 12 : 17 – 21
17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
18 Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Isaya 26 : 21
21 Kwa maana, tazama, BWANA anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.

Ufunuo 19 : 11 – 21
11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama muali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililoloweshwa katika damu, na jina lake anaitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili kwa upanga huo awapige mataifa. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.
17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njooni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.
19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake.
20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao hao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wakiwa hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;
21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.

Ufunuo 20 : 15
15 Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Zaburi 75 : 8
8 ④ Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.

Warumi 6 : 23
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Mathayo 7 : 13 – 14
13 ⑱ Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 ⑲ Bali mlango ni mwembamba, na njia imebana iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Ezekieli 25 : 17
17 Nami nitajilipiza kisasi kikuu, nikiwakemea kwa ukali; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapojilipiza kisasi juu yao.

Nahumu 1 : 2 – 6
2 BWANA ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; BWANA hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.
3 BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
4 Yeye huikemea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote; Bashani hulegea, na Karmeli; nalo ua la Lebanoni hulegea.
5 Milima hutetema mbele zake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele za uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake.
6 Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.

Mathayo 10 : 28
28 ⑤ Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.

2 Petro 2 : 9
9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;

Waraka kwa Waebrania 9 : 22
22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.

Kumbukumbu la Torati 9 : 7
7 Kumbuka, usisahau ulivyomtia BWANA, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hadi mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya BWANA

Zaburi 7 : 11
11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu akasirikiaye waovu kila siku.

Luka 12 : 5
5 Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanamu; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.

Wagalatia 5 : 19 – 21
19 ⑬ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi,
21 ⑭ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Wagalatia 2 : 20
20 ① Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

Luka 10 : 1 – 456

1 Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda katika kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.
2 Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini wafanya kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke wafanya kazi katika mavuno yake.
3 Nendeni, angalieni, nawatuma kama wana-kondoo kati ya mbwamwitu.
4 Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani.
5 Na nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu;
6 na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; lakini kama hamna, amani yenu itarudi kwenu.
7 Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mfanya kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihamahame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
8 Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu;
9 waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.
10 Na mji wowote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni,
11 Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.
12 Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo.
13 Ole wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakikaa katika nguo za magunia na majivu.
14 Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi.
15 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
16 Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.
17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.
18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.
19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.
21 Saa ile ile alishangilia katika Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza.
22 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
23 Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi.
24 Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.
25 Na tazama, mwanasheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?
27 ① Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
28 ② Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.
29 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?
30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakamwacha akiwa karibu kufa.
31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.
33 ③ Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipokuwa; na alipomwona alimhurumia,
34 akakaribia, akamfunga majeraha yake, akayatia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na chochote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?
37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Nenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.
38 ④ Ikawa katika kuenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake.
39 Naye alikuwa na dada yake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.
40 Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo dada yangu alivyoniacha nifanye kazi peke yangu? Basi mwambie anisaidie.
41 Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;
42 ⑤ lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hatanyang’anywa.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *