Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Gaza
Yoshua 13 : 3
3 kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
Yeremia 25 : 20
20 na watu wote waliochanganyika pamoja, na wafalme wote wa nchi ya Uzi, na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi;
Mwanzo 10 : 19
19 ⑬ Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.
Kumbukumbu la Torati 2 : 23
23 ⑱ na Waavi waliokuwa wakikaa katika vijiji mpaka Gaza waliangamizwa na Wakaftori waliotoka Kaftori, na hawa wakakaa badala yao.)
Yoshua 11 : 22
22 ⑱ Hawakusalia Waanaki hata mmoja katika nchi ya wana wa Israeli; isipokuwa walisalia katika Gaza, na katika Gathi, na katika Ashdodi.
Yoshua 15 : 47
47 ④ Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kuu na pwani yake.
Waamuzi 1 : 18
18 Pamoja na haya Yuda aliutwaa Gaza pamoja na mipaka yake, na Ashkeloni na mipaka yake, na Ekroni na mipaka yake.
Waamuzi 16 : 23
23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.
Waamuzi 16 : 31
31 Ndipo ndugu zake, na watu wote wa nyumba ya baba yake wakateremka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.
1 Wafalme 4 : 24
24 ⑱ Kwani alikuwa akitawala nchi yote upande huu wa Mto, toka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa Mto; naye alikuwa na amani pande zake zote.
Yeremia 47 : 1
1 Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza.
Amosi 1 : 7
7 lakini nitatuma moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake.
Sefania 2 : 4
4 Kwa kuwa Gaza utaachwa, na Ashkeloni utakuwa ukiwa; wataufukuzia mbali Ashdodi wakati wa adhuhuri, na Ekroni utang’olewa.
Zekaria 9 : 5
5 ⑩ Ashkeloni ataona haya na kuogopa; Gaza pia, naye atafadhaika sana; na Ekroni, kwa maana matarajio yake yatatahayarika; na mfalme ataangamia toka Gaza, na Ashkeloni atakuwa hana watu.
Matendo 8 : 39
39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.
Leave a Reply