Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ethan
1 Wafalme 4 : 31
31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.
Zaburi 89 : 1
1 Fadhili za BWANA nitaziimba milele; Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 6
6 ⑥ Na wana wa Zera; Zabdi, na Ethani, na Hemani, na Kalkoli, na Darda; hao wote ni watano.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 8
8 Na wana wa Ethani; Azaria.
1 Mambo ya Nyakati 6 : 42
42 mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei;
1 Mambo ya Nyakati 6 : 44
44 Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki;
1 Mambo ya Nyakati 15 : 17
17 ⑯ Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana wa Kishi;
1 Mambo ya Nyakati 15 : 19
19 Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;
Leave a Reply