Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Eshkoli
Mwanzo 14 : 13
13 Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; aliyekuwa akikaa karibu na mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.
Mwanzo 14 : 24
24 isipokuwa hivyo walivyokula vijana, na sehemu za watu waliokwenda nami, yaani, Aneri, na Eshkoli, na Mamre; na watwae wao sehemu zao.
Hesabu 13 : 24
24 Bonde lile liliitwa bonde la Eshkoli[24] kwa sababu ya hicho kishada walichokata huko wana wa Israeli.
Hesabu 32 : 9
9 ⑥ Kwa kuwa walipokwea na kuingia bonde la Eshkoli, na kuiona nchi, wakawavunja mioyo wana wa Israeli, ili wasikwee kuingia nchi aliyowapa BWANA.
Kumbukumbu la Torati 1 : 24
24 Nao wakageuka, wakapanda mlimani wakafika katika bonde la Eshkoli, wakalipeleleza.
Leave a Reply