Biblia inasema nini kuhusu adhabu kwa uzinzi – Mistari yote ya Biblia kuhusu adhabu kwa uzinzi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia adhabu kwa uzinzi

Mithali 6 : 32
32 ⑭ Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

Mambo ya Walawi 20 : 10
10 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mwanamume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.

Kumbukumbu la Torati 22 : 22
22 Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli.

1 Wakorintho 6 : 9
9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,

Yohana 8 : 3 – 11
3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
5 ⑧ Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake kama hawa; nawe wasemaje?
6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika ardhi.
7 ⑩ Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika ardhi.
9 ⑪ Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
10 Yesu akainuka asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
11 ⑫ Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Nenda zako; wala usitende dhambi tena.]

Yakobo 4 : 17
17 Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

Warumi 10 : 13
13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.

Waraka kwa Waebrania 13 : 4
4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

Malaki 2 : 16
16 Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.

Luka 16 : 18
18 Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.

Mambo ya Walawi 20 : 13
13 ① Tena mwanamume akilala pamoja na mwanamume, kama alalavyo na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.

Mathayo 25 : 46
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

1 Petro 3 : 18
18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; akauawa kimwili, lakini akahuishwa kiroho,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *