Biblia inasema nini kuhusu Edomu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Edomu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Edomu

Mwanzo 25 : 25
25 Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.

Mwanzo 25 : 30
30 Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.[11]

Mwanzo 36 : 1
1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ndiye Edomu.

Mwanzo 36 : 8
8 Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu.

Mwanzo 36 : 19
19 Hao ni wana wa Esau, na hao ndio majumbe wao; naye Esau ndiye Edomu.

Mwanzo 32 : 3
3 ② Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.

Mwanzo 36 : 17
17 Na hawa ni wana wa Reueli, mwanawe Esau; jumbe Nahathi, jumbe Zera, jumbe Shama, jumbe Miza. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Basemathi, mkewe Esau.

Mwanzo 36 : 21
21 na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, wana wa Seiri, katika nchi ya Edomu.

Yeremia 40 : 11
11 Kadhalika waliposikia Wayahudi wote, waliokuwa katika Moabu, na kati ya wana wa Amoni, na hao waliokuwa katika Edomu, na hao waliokuwa katika nchi zote, ya kuwa mfalme wa Babeli amewaachia Yuda mabaki, na ya kuwa amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, juu yao;

Obadia 1 : 8
8 Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema BWANA.

Obadia 1 : 14
14 Wala usisimame penye njia panda, ili kuwakatilia mbali watu wake wakimbiao; wala usiwatoe watu wake waliosalia, katika siku ya dhiki.

Yeremia 25 : 23
23 Dedani, na Tema, na Buzi, na watu wote wakatao denge;

Yeremia 27 : 11
11 Bali taifa lile watakaotia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, na kumtumikia, taifa hilo nitawaacha wakae katika nchi yao wenyewe, asema BWANA; nao watailima, na kukaa ndani yake.

Isaya 63 : 1
1 ④ Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *