Biblia inasema nini kuhusu dhambi isiyosameheka – Mistari yote ya Biblia kuhusu dhambi isiyosameheka

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia dhambi isiyosameheka

Marko 3 : 28 – 29
28 Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;
29 bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,

Luka 12 : 10
10 Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Mtu atasamehewa, bali aliyemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.

Mathayo 12 : 31 – 32
31 ⑱ Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.
32 ⑲ Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

1 Yohana 5 : 16 – 18
16 ⑦ Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.
17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
18 ⑧ Tunajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.

Mathayo 12 : 32
32 ⑲ Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

Mathayo 12 : 31
31 ⑱ Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.

Waraka kwa Waebrania 10 : 26
26 ⑬ Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;

1 Yohana 5 : 16
16 ⑦ Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.

1 Yohana 1 : 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.

1 Timotheo 1 : 13
13 ingawa hapo awali nilikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye ujeuri, lakini nilipata rehema kwa kuwa nilifanya hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.

Waraka kwa Waebrania 6 : 4 – 8
4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za wakati ujao,
6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumtweza hadharani kwa dhahiri.
7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao inalimwa, hupokea baraka zitokazo kwa Mungu;
8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.

Marko 3 : 28 – 30
28 Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;
29 bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,
30 kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *