Biblia inasema nini kuhusu Dawa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Dawa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Dawa

Mithali 17 : 22
22 Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.

Isaya 1 : 6
6 Toka wayo wa mguu hadi kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwazongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta.

Isaya 38 : 21
21 Maana Isaya amesema, Na watwae mkate wa tini, wakauweke juu ya jipu, naye atapona.

Yeremia 8 : 22
22 ③ Je! Hakuna marhamu katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?

Yeremia 30 : 13
13 Hapana mtu wa kukutetea; kwa jeraha lako huna dawa ziponyazo.

Yeremia 46 : 11
11 ⑯ Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.

Yeremia 51 : 9
9 ③ Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni.

Ezekieli 47 : 12
12 Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayataisha kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa.

Luka 10 : 34
34 akakaribia, akamfunga majeraha yake, akayatia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *