Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Daniel
Danieli 2 : 49
49 ④ Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya utawala wa Babeli; lakini huyo Danieli alikuwa akikaa katika lango la mfalme.
Danieli 5 : 11
11 ⑭ Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadneza, baba yako, naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu;
Danieli 5 : 29
29 Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.
Danieli 6 : 2
2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili wakuu hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
Danieli 4 : 9
9 Ee Belteshaza, mkuu wa waaguzi, kwa sababu ninajua ya kuwa roho ya miungu watakatifu[2] inakaa ndani yako, na ya kuwa hapana neno la siri likushindalo, niambie maana ya hii ndoto yangu niliyoiona, na tafsiri yake.
Mathayo 24 : 15
15 Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
Danieli 1 : 16
16 Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu.
Danieli 1 : 17
17 Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
Ezekieli 28 : 3
3 ⑰ Tazama, una hekima kuliko Danieli; hapana neno la siri watu wawezalo kukuficha;
Danieli 2 : 18
18 ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kuhusu siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli.
Danieli 12 : 13
13 Lakini nenda zako hata utakapokuwa mwisho ule; maana wewe utastarehe, nawe utaamka katika kura yako mwisho wa siku hizo.
Ezekieli 14 : 14
14 wajapokuwa watu hawa watatu, Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao, asema Bwana MUNGU.
Leave a Reply