Biblia inasema nini kuhusu Zereshi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Zereshi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Zereshi

Esta 5 : 14
14 Basi Zereshi mkewe na marafiki wote wa Hamani wakamwambia, Na kitengenezwe kiunzi cha mti wa kunyongea wa urefu wa mikono hamsini, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa furaha pamoja na mfalme karamuni. Basi ushauri huu ukamridhisha Hamani, akautengeneza mti wa kunyongea.

Esta 6 : 13
13 Basi Hamani akawasimulia Zereshi mkewe na marafiki zake wote kila neno lililompata. Kisha watu wake wenye hekima na Zereshi mkewe wakamwambia, Ikiwa huyu Mordekai, ambaye umeanza kuanguka mbele yake, ni wa uzao wa Wayahudi, wewe hutamweza, bali kuanguka utaanguka mbele yake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *