Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yuda
Mathayo 10 : 4
4 Simoni Mkananayo, na Yuda Iskarioti, naye ndiye aliyemsaliti.
Marko 3 : 19
19 na Yuda Iskarioti, ndiye aliyemsaliti. Kisha akaingia nyumbani.
Luka 6 : 16
16 na Yuda wa Yakobo, na Yuda Iskarioti, ndiye aliyekuwa msaliti.
Matendo 1 : 17
17 kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, akapata sehemu ya huduma hii.
Yohana 12 : 6
6 Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwizi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
Yohana 13 : 29
29 Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu.
Yohana 12 : 6
6 Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwizi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
Mathayo 26 : 16
16 Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi apate kumsaliti.
Marko 14 : 11
11 Nao waliposikia walifurahi, wakaahidi kumpa fedha. Akatafuta njia ya kumsaliti wakati wa kufaa.
Luka 22 : 6
6 Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.
Yohana 13 : 2
2 Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, moyo wa kumsaliti;
Yohana 17 : 12
12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi niliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
Mathayo 26 : 50
50 Yesu akamwambia, Rafiki, fanya ulilolijia. Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu.
Marko 14 : 45
45 Basi alipokuja, mara akamwendea, akasema, Rabi, akambusu.
Luka 22 : 49
49 Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotokea, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga?
Yohana 18 : 5
5 Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
Matendo 1 : 25
25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe.
Mathayo 27 : 10
10 wakavitumia kwa kununua shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.
Leave a Reply